Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA UBUNGE WA UKAWA KAHAMA MJINI JAMES LEMBELI AANZA KUTEMA CHECHE



Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kati wilaya ya Kahama kimesema hakita kuwa tayari kuona watendaji wa manispaa ya Kahama ikiwanyanyasa wafanyakazi wa serekali kwa kuwa cheleweshea stahiki zao kama walimu, polisi, idara ya afya, na mahakama.


Mgombea ubunge kwa tiketike Chadema Bwana James Lembeli ambaye aliingia kwa usafiri wa helkopta amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaomba wakazi wa mji wa Kahama kumpigia kura mgombea urais, ubunge na madiwani wa UKAWA. 


Awali mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mara Bwana Vincent Nyerere aliyekuwa akimnadi mgombea urais Bwana Edward Lowassa amesema endapo wananchi wakiwachagua wagombea wa UKAWA watumishi wa serekali hawata kuwa na malimbikizo ya madeni ambayo wanaidai serikali.

Mamia ya wakazi wa mji wa Kahama na vitongoji vyake walikuwa wakimkatisha mara kwa mara mgombea ubunge wa Kahama mjini kwa kumshangilia, Bwana Lembeli ambaye ameweza kufanya mikutano sita katika vijiji tofauti kwa siku moja kwa kutumia usafiri wa helkopta.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com