Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA URAIS WA UKAWA ALAZIMIKA KUAHIRISHA KUFANYA MKUTANO HUKO TANGA




Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga.


Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8 zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo.

Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.


Umati huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili ulionekana dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya msalaba mwekundu redcross mjini Tanga.

Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.


 SOMA TAARIFA KAMILI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com