Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA ATIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM




Watanzania wametakiwa kutokukubali kuhadaika na ahadi zinazotolewa na baadhi wa wagombea katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu kwani wengi wao hawana dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo hapa nchini.

Akiwa jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Kagera, Mh.Edward Lowassa bado dhamira yake ni ileile ya kuleta maendeleo hapa nchini.


Katika mikutano mikubwa ya hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti na kuhudhuliwa na maelf ya wakazi wa jijini Dar es Salaam amesema serikali yake ya awamu ya tano itajikita katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wanyonge ambao wameshindwa kunufaika na rasmilini za nchi kwa miaka 50 iliyopita.


Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu anasema watanzania hawapaswi kudhoofishwa na baadhi ya kauli za vitisho na kuwataka kufanya maamuzi kwani nchi itakuwa salama kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Mh.Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA amefanya mikutano katika jimbo la Ukonga, jimbo la Kigamboni kabla ya kufanya mkutano mkubwa uliohudhuliwa na maelf ya wakazi kutoka pande zote za jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com