
Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwa na viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamika kama ilivyo sasa unabaki kuwa historia.

Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma za kijamii ikiwemo elimu aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri mkuu.
Mheshimiwa Lowassa akizungumza

Awali waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lisu wamesema kukithiri kwa malalamiko ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa kuchukua hatua wakiendelea kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao wa kupata ufumbuzi umefika mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya kuondoa tatizo hilo.
Wananchi na viongozi wa jimbo la Mtera wamesema ubinafsi wa viongozi wa CCM, na ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya kuondokana na umaskini hasa kwa vijana suala ambalo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira Dr Makongoro Mahanga ambaye sasa amehamia UKAWA alipata fursa ya kulitolea ufafanuzi.
Lowasa katika viwanja vya BARAFU Dodoma leo ameweka Historia katika mkutano huo kwa umati mkubwa wa watu uliojitokeza kumlaki na kumsikiliza.
Baada ya mkutano kumalizika wananchi hawakuridhika wakaamua kumsindikiza hadi nyumbani kwake Dodoma na umati mkubwa sana uliwasili nyumbani kwake wakifwatana na msafara wake jambo ambalo halikuwahi kutokea kwa mgombea mwingine katika mji huo ambao ni mji mkuu wa Tanzania
Akihitimisha mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika Dodoma mjini Mh Lowaasa ambaye sasa anaelekea mkoa wa Singida ameendelea kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa wakati na kwakasi inayostahili.

Social Plugin