MWALIMU KAAMUA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE MWENYE MIAKA CHINI YA 16..ADHABU YAKE HII HAPA
Thursday, September 24, 2015
Nchi nyingi duniani kote ikiwemo Tanzania sheria ya mtu kuvuka umri wa kuitwa mtoto, hadi afikishe umri wa miaka 18 na kuendelea ndio inaaminika kuwa ni mtu mzima, ila mtu aliye chini ya miaka 18 haruhusiwi kutumia vitu kadhaa kama pombe, kujihusisha katika mahusiano ya kimapenzi hususani na mtu aliyemzidi umri.
Caroline Berriman
Licha ya kukiri kufanya kosa la kutembea na mwanafunzi wake mwalimu Caroline Berriman amehukumiwa kwenda jela. Caroline Berriman ambaye alikuwa ni mwalimu wa darasa msaidizi katika shule ya Abraham Moss Community, alishitakiwa kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi wake aliye na umri wa miaka 16.
Caroline Berriman ambaye ana umri wa miaka 30 kwa sasa, alishitakiwa kwa makosa mawili ya kufanya mapenzi na mtoto na kutenda kosa hilo katika sehemu inayoaminiwa na watu.
Caroline Berriman ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya Abraham Moss Community iliyoko jijini Manchester, shule ambayo ina wanafunzi 1600 wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 16 wa shule ya msingi na sekondari, amehukumiwa kwenda jela miaka miwili, kufanya kazi za kijamii za bila malipo kwa muda wa masaa 250 pamoja na kulipa pound 100 kama fidia kwa muhanga.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin