Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI ndugu Peter Elias ametimuliwa kutoka msafara wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Magufuli, imethibitishwa.
Mwandishi huyo ametimuliwa kwa kosa la kuripoti tukio la mgombea huyo kuzomewa na wafuasi wa Chadema jijini Mbeya hivi karibuni kinyume cha makubaliano.
Mwandishi huyo aliripoti katika gazeti hilo kwa kichwa cha habari "Magufuli akabiliana na UKAWA Mbeya" na kuweka picha ya mgombea huyo akionyeshwa alama ya vidole viwili.
Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuzuiwa kufanya kazi yao kwa kile kilichodaiwa kuwa hawapo kwenye msafara wa Magufuli....
SOMA HABARI YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUINGILIWA UHURU WAO MKUTANO WA MAGUFULI HAPA
Social Plugin