Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

News Alert!! EMMANUEL MBASHA ASHINDA KESI UBAKAJI.....SASA YUKO HURU







Emmanuel Mbasha akiwa amepiga magoti huku akitokwa machozi nje ya Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam baada ya Hukumu kutolewa.-Picha na Millardayo.com




Mahakama ya Ilala, Dar imemwachia huru Emmanuel Mbasha leo Jumatatu Septemba 21, 2015 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la ubakaji dhidi yake.


Itakumbukwa mwaka 2014 Emmanuel Mbasha ambae ni mwimbaji wa injili na mfanyabiashara alifunguliwa mashtaka mawili mahakama ya Ilala kwa makosa mawili ikiwemo la ubakaji.


Katika shitaka la kwanza Mei 23, mwaka 2014 eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, ilidaiwa kinyume cha sheria alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake.


Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka 2014 eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake.




Mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ambaye alikuwa na tuhumu za kesi ya kumbaka shemeji yake…baada ya kuachiwa huru amefunguka na kusema Mungu ni mwema ameshinda kesi, anamshukuru sana Mungu, anawashukuru Watanzania wote kwa kumuombea kwa kuwa alikua kwenye mapito magumu sana katika maisha yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com