Wananchi wa wilaya Nzega mkoani Tabora wamewataka watanzania wanaotaka mabadiliko ya kweli wamesema kabla ya CCM na serikali yake kutaka kuendelea kutawala wana deni kubwa la kuwaeleza watanzania kinachosababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma kama elimu maji na afya huku wengine wakinufaika wakati wote wanalipa kodi iliyo sawa.
Wakiwa kwenye viwanja vya polisi Nzega mkoani Tabora wananchi hawa wanasema licha ya kuendelea kuelezwa maneno yasiyo na vitendo ni jambo lililoko wazi kuwa CCM imeshindwa kusimamia uwiano kinachotoka serikalini kwenda wananchi na kinachotoka kwa wananchi kwenda serikalini na ndio sababu sasa wanataka mabadiliko.
Katika maeneo mbalimbali ilikofanyika mikutano ya kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA baadhi ya viongozi wanaounga mkono vuguvugu la mabadiliko wamesema licha ya changamoto zilizopo wataendelea kusimamia mabadiliko kuwaeleza watanzania maovu yanayoendelea kufanyika.
Mgombea urais wa vyama vinavyounda ukawa Mh Edward Lowassa baada ya kufanya mikutano katika majimbo ya Igunga na Sikonge akamalizia mkutano wa mwisho kwa kuendelea kumwaga sera kwa wananchi wa Nzega kwa kuwataka watanzania kutafakari kwa kina changamoto zinazowakabili na kuamua kuziepuka kwa kuchagua viongozi wa UKAWA.