PICHA- KUHUSU TUKIO LA MOTO KUTEKETEZA NYUMBA MJINI SHINYANGA,MPANGAJI AHUSISHWA


Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa karibu na nyumba iliyoteketea kwa moto katika mtaa wa Moleka Kata ya Ngokolo karibu na stendi ya mabasi mjini Shinyanga leo asubuhi.Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni jiko la mkaa lililoachwa ndani ya chumba cha mmoja wa wapangaji 7 (aliyejulikana kwa jina la Veronica/Mama Junior) katika nyumba ya Kashinje Masaka,ambaye sasa anaishi Isaka wilayani Kahama lakini msimamizi wake Mwashi Kashinje aliyekuwa anaishi na wapangaji hao.Picha zote na Suzy Butondo- Malunde1 blog Shinyanga


Askari wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga wakizima moto huo .Hata hivyo pamoja na kufanikiwa kuzima moto huo vitu vyote ndani ya nyumba hiyo ambavyo havijajulikana thamani yake vilikuwa vimeshateketea kwa moto



Mwendesha baiskeli maarufu Daladala akiondoka eneo la tukio kutokana na moshi mkubwa katika eneo hilo


Mtoto wa mwenye nyumba Mwashi Kashinje, amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu na nusu asubuhi wakati wakifanya usafi, ambapo ghafla akaona moto unalipuka kutoka kwenye chumba cha mpangaji ambaye walikuwa wamempatia notes ya kuondoka kutokana na tabia zake mbaya ikiwemo kutolipa bili za umeme.



Nyumba ikiteketea kwa moto....Kashinje ambaye ni msimamizi wa nyumba hiyo amesema baada ya kuona moto huo umelipuka akakimbilia kuzima swichi kuu ya umeme lakini moto huo tayari ulikuwa umeshashika kasi na hivyo kuchukua watoto wote na kukimbilia nje kwa ajiri ya kuomba msaada kwa wasamaria wema kuuzima moto huo.


Amesema katika nyumba hiyo anaishi na wapangaji saba ambapo tangu mwezi Agosti mwaka huu mpangaji mmoja anayejulikana kwa jina la Veronica au Mama Junior alimpa notes ya kuondoka baada ya tabia yake kuwa mbaya, lakini mpangaji huyo alitamka kuwa lazima afanye kitu kibaya kwenye nyumba hiyo.


Mashuhuda wa tukio hilo waamesema chanzo cha moto huo huenda ni jiko la mkaa lililokutwa likiwaka ndani ya chumba cha mpangaji huku juu kukiwa na sufuria na kwamba baada ya moto huo kulipuka alitoka mwanamme ndani ya chumba cha mpangaji ambaye hakujulikana ni nani kutokana na kwamba mpangaji huyo ana tabia ya kuingia na wanaume wa kila aina katika chumba chake.


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema wanafanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo cha moto huo na ikibainika kuwa mpangaji huyo kahusika watamchukulia hatua kali za kisheria.

Picha zote na Suzy Butondo- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post