Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha zaidi ya 50 !! MAFURIKO YA HATARI YA LOWASSA HUKO BUKOBA,NI BALAA MTUPU


Umati wa Wananchi wa Mji wa Bukoba ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Aghakhan kuhudhulia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 19, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi Bukoba waliofika kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadhi ya wagombea wa Udiwani wa vyama vinavyouda UKAWA, kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mmoja wa wadau wa Mabadiliko, Prof. Azaveli Rwaitama, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza, Mh. Ezeckiel Wenje akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, akimuombea Mumewe Kura kwa Wananchi wa Mji wa Bukoba, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimpongeza Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Bukoba.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Aliekuwa Meya Mji wa Bukoba, Anatory Amani akizungumza kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.








Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza na baadhi ya vingozi, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi, Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Wananchi wa Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye eneo la Mkutano.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Nkenye, Misenyi Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Bw. Simon Andrew (55) ambaye ni Mlemavu wa miguu, mkazi wa Kijiji cha Kilimilile, Kyaka Wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera leo Septemba 19, 2015.

Picha zote zimepigwa na Othman Michuzi kutoka Michuzi Media.



Mgombea urais wa ukawa Mh.Edward Lowasa amesema UKAWA ikipata nafasi ya kuwaongoza watanzania itahakikisha maziwa na mito mikubwa ukiwemo mto Kagera inatumika kuondoa matatizo yanayochangia wananchi kuwa maskini likiwemo la maji,njaa na ukosefu wa kipato.





Akizungumza na wananchi waliofurika katika mikutano iliyofanyika majimbo ya Nkenge,Bukoba vijijini na Bukoba mjini Mh.Lowasa pia amesema serikali atakayounda itahakikisha tatizo la usumbufu wa wananchi wanaoishi mipakani libaki kuwa historia.

Mh.Lowasa ambaye amesema hana muda wa kuwajibu wanaoendelea kumsakama pia ametoa ufafanuzi wa zitakapopatikana fedha za kulipia elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa kusema kuwa atatumia fedha zinazotumika sasa kwenye safari za viongozi zisizo za lazima ,semina na makongamano,na ununuzi wa magari ya kifahari.




Baadhi ya makada na wagombea wa UKAWA wameendelea kuweka wazi matatizo yanayochangiwa na udhaifu CCM na jinsi UKAWA ilivyojipanga kupitia sera zilizoko kwenye ilani yake kuondoa udhaifu huo.
Mh.Lowasa amemaliza kampeni katika mkoa wa Kagera na mchakamchaka wa kunadi sera sasa unaelekea jijini Dar es Salam na hatmaye mikoa ya Kusini.






















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com