TRENI YA ABIRIA YAACHA NJIA SHINYANGA,ABIRIA ZAIDI YA 150 WANUSURIKA KUFA




Hapa ni katika eneo la station mjini Shinyanga treni ya abiria ikiwa imeacha njia( haionekani vizuri hapo chini) na kusababisha abiria 159 waliokuwa wanasafiri na treni hiyo kutoka Tabora kwenda jijini Mwanza kunusurika kufa na kukwama kwa saa kadhaa.Picha zote na Suzy Butondo -Malunde1 blog Shinyanga 


Tukio hilo limetokea leo asubuhi baada ya kichwa cha treni hiyo kutoka kwenye njia ya reli na mabehewa ya treni kuanza kukanyaga mataluma na kusababisha adha kwa abiria hao.


Mkuu wa kituo cha reli (Station Master) Shinyanga Baruani Issa amesema katika treni hiyo kulikuwa na abiria 159 na kwamba ajali hiyo imetokea kutokana na miundo mbinu ya reli kuwa chakavu. 



Station Master huyo amesema utaratibu uliofanywa na Shirika hilo ni kufanya utaratibu wa kuwarudishia nauli abiria hao ili wapande mabasi na kuendelea na safari zao ili kupunguza usumbufu wakati utaratibu wa matengenezo unafanyika ili treni iendelee na safari zake kama kawaida.

Wakizungumza na Malunde1 blog abiria waliokuwa wanasafiri na treni hiyo mbali na kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuwanusuru na ajali hiyo wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu ya reli kwani asilimia kubwa ya Watanzania wanategemea usafiri huo wenye gharama nafuu.

Picha zote na Suzy Butondo- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post