TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YATANGAZA MAJINA 14 YA WAGOMBEA URAIS




Tume ya uchaguzi ya Zanzibar imewapitisha wagombea kutoka vyama 14 kugombea urais wa Zanzibar katika uchagzui mkuu mwezi wa Oktoba mwaka huu.


Akitangaza uamuzi huo wa tume mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Salum Kassim Ali amesema tume imeridhika na wagombea hao wakiwemo CCM, CUF na TADEA na sasa na majina hayo yatabandikwa nje kwa masaa 24 ili kama kutakuwa na pingamizi watapitia na kutolea maamuzi ndani ya masaa 24.

Mapema wagombea wa vyama 10 kati ya 11 waliobaki walikamilisha utaratibu wa tume ya kuwasilisha fomu na ada ya shilingi milioni mbili huku mgombea wa mwisho wa chama cha NRA Seif Ali Iddi aliwasilisha fomu zake kukiwa kumesalia dakika 3 bada ya kupata ajali akiwa njiani kuja ofisi za tume, hata hivyo alifanikiwa na tume kumpokea na jina lake kubandikiwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Wagombea wengine waliofika wakati wa asubuhi katika ofisi za tume ni pamoja na mgombea wa chama cha Jahazi asilia Kassim Bakari Ali ambaye alifika akiwa katika gari maalum na baadaye akafuata mgombea wa ADC Bw Hamad Rashid akiwa ameonganzana na wafuasi wa chama hicho ambapo wagombea wote hao walilia haki na huru katika uchaguzi mkuu.

Kampeni za urais wa Zanzibar zinatarajiwa kuanza rasmi kuanzia jumatatu jioni huku kukiwa hakuna dalili ya kuwepo pingamizi kutoka kwa mgombea yeyote, zoei hilo limeshudia wagombea 15 wakijitokeza kuwania urais wa Zanzibar mwaka huu tafauti na uchagzui ulipita walikuwa wagombea saba, chama pekee ambacho kimeshindwa kurejesha foumu ni cha UPDP ambaye mgombea wake alikuwa mwanamke Mwajuma Ali Khamis.

Via>>>Itv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post