Usiku wa September 24 2015 taarifa ya Majonzi imesambaa na kuwafikia watu kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya Kijamii, Serikali ikathibitisha pia kuhusu msiba wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mama Celina Kombani amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani, na amefariki akiwa India ambako alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kuhusu taratibu zinazofatia, nimeipata taarifa kutoka Ofisi za Bunge ambapo inaonesha mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu mpaka Dar es Salaam inafanyika na mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar Jumatatu September 28 2015, na baadae msiba utasafirishwa kupelekwa Mahenge Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mazishi.
Marehemu Mama Celina Kombani amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na alikuwaWaziri na pia Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki.
RIP Mama Celina Kombani.
Social Plugin