MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vinavyounda Ukawa,Edward Lowassa amezidi pasua anga ndani ya nchi,
baada ya leo kutikisa mkoani Dodoma na kushuhudiwa na maelfu ya wakazi wa mkoa huo.
Katika Kampeni hizo zinazoendelea, Lowassa amewataka Watanzania kutofanya makosa tena ya kuchagua chama kingine isipokuwa UKAWA .
Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameanza kumwaga sera za mabadiliko zilizoko kwenye ilani ya umoja huo katika mkoa wa Dodoma na amewataka watanzania kuiwezesha UKAWA kuingia madarakani ili waanze kazi ya kuondoa kero za wananchi zilizoshikana chini ya utawala wa CCM kutokana mfumo kandamizi zikipata ufumbuzi kwa muda mfupi likiwemo tatizo la maji.
Kama ilivyokuwa katika maeneo mengine aliyopita Mh Lowassa ameendelea kupata mapokezi makubwa ya wananchi wakitaka kusikia sera na jinsi wanavyoweza kuondokana na matatizo yanayowakabili.
Tatizo la maji ni miongoni mwa yanayolalamikiwa kwa muda mrefu na asilimia kubwa ya watanzania wakiwemo wa mikoa ya kanda ya kati ambalo, wananchi hawa wa Gairo ambao ni sehemu kidogo ya watanzania wanaolalamikia wanathibitisha.
Mh Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA wanaweka wazi jinsi walivyojipanga kulikabili na hata kulimaliza tatizo hilo na mengoine mengi kupitia sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA.
Tatizo la udhaifu wa katiba na usimamizi wa sheria ni miongoni mwa mambo yanayoelezwa na viongozi waandamizi wa UKAWA akiwemo Mh Tundu Lisu kuchangia umasikini unaowakabili wananchi.
Mh lowassa bado anaendelea kunadi sera za UKAWA katika majimbo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamia mikoa ya Singida naShinyanga.