Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKATI WATU WANAJADILI UTAFITI WA TWAWEZA, LEO LOWASSA AZIDI KUFANYA MAAJABU HUKO MTAWARA, SHUHUDIA MAFURIKO YAKE HAPA


Wakazi wa mji wa Mtwara wamemhakikishia mgombea wa nafasi ya urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edward Lowassa kuwa wamejipanga kumpigia kura nyingi zitakazomuwezesha kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu,
Saa chache baada ya taasisi ya kitafiti ya Twaweza kuweka hadharani na matokeo ya utafiti kuwa CCM na Magufuli ndiyo wanapendwa zaidi na wananchi
Awali akihutubia maelfu ya wakazi wa jimbo la Masasi na viunga vyake mgombea wa nafasi ya urais Mh.Edward Lowassa amewaahidi wakazi wa kusini kuwaboreshea mazingira ya kiuchumi huku akiwahakikishia kuondosha kero ya stakabadhi gharani ambayo imekuwa ikiwa nyongonyesha wakulima wadogo.

Timu ya kampeni iliyochini ya mgombea wa nafasi ya urais, wamewataka wananchi Mtwara kusini kwa ujumla kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi kwani kushindwa kufanya hivyo ni kuendelea kupokonywa rasilimali ambazo zinakwenda kuneemesha mahali kwingine.

Mh.Edward Lowassa amehitimisha ziara yake katika mkoa wa Mtwara baada ya kufanikiwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa miji ya Newala, Tandahimba, Mtwara mjini, Ndanda kabla ya kuhitimisha katika uwanja bomani mjini Masasi, ambapo kesho anatarajiwa kuanza kuunguruma katika viunga tofauti mkoni Lindi.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com