Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE WAGEUZWA "MAABARA" HUKO SUMBAWANGA




Mshauri wa jinsia wa Shirika la Plan International Bi. Jane Mrema



Baadhi ya wananchi wa vijiji katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wamelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wanaume vya kuwageuza wenza wao kuwa maabara, kwa kuwatanguliza kwenye vituo vya afya,na kisha kuyafanya matokeo ya vipimo kama yao.





Wananchi hao kutoka katika vijiji vya msia, kinambo, kisa na milepa wengi wao wakiwa ni wahudumu wa afya vijijini , wamesema wakati umefika badala ya wanaume kuwaacha wake zao kuyachukua matokeo ya vipimo vya afya walivyopima na kuvifanya ni vya yao pia kwa kuamini kuwa majibu ya wenza wao yanafanana na yao.







Aidha Wananchi hao wameongeza kuwa Wanaume kwa sasa wanapaswa wawasindikize wenza wao wakati wote wa ujauzito na kupima afya na tabia hiyo iwe endelevu na sio wakati wa Ujauzito tu
Akiongea na wananchi hao , Mshauri wa jinsia wa Shirika la Plan International Bi. Jane Mrema, ametoa wito kwa wanaume wote waliobadilika na kuukimbia mfumo dume ndani yao, wasifanye hivyo wakati wenza wao wakiwa wajawazito pekee, bali wafanye usaidizi huo kuwa endelevu kwa ajili ya kuwapunguzia wanawake mzigo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com