Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUHUMIWA 10 WA MAUAJI YA MKULIMA NA NG'OMBE 68 HUKO MOROGORO WAKAMATWA


Siku chache baada ya mkulima mmoja kuuwawa kikatili na Ng’ombe 68 kuuawa katika kijiji cha Tindiga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro jeshi la polisi limewashikilia watuhumiwa 10 wakiwemo wafugaji waliohusika na mauaji na wakulima waliohusika kukatakata Ng’ombe.



Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema watuhumiwa wawili waliohusika na mauaji ya mkulima mmoja tayari wamefikishwa mahakamani na wengine nane waliohusika kuuwa Ng’ombe 68 na wengine kukatwa katwa na mapamnga wanashikiliwa na jeshi hilo na watafikishwa mahakamani ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Morogoro wakizugumzia tukio hilo la mauaji ya watu na mifugo wameishauri serikali kuona umuhimu wa kutenganisha maeneo ya kilimo na ufugaji katika vijiji vya wakulima na wafugaji kwa lengo la kuepusha mauaji na kurejesha hali ya amani na utulivu katika wilaya za Kilosa na Mvomero ambako migogoro hiyo inaendelea mara kwa mara na kugharimu maisha ya wananchi na mifugo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com