NIMEKUWEKEA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA LEO. YANGA MAFURIKO
Saturday, September 19, 2015
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena September 19 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, mechi ambazo zimechezwa September 19 ni mechi nne, klabu ya Yanga imeikaribisha klabu ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa taifa Dar Es Salaam, huku Stand United ya Shinyanga ikiwa mwenyeji wa African Sports ya Tanga.
Mgambo Shooting imeikaribisha Maji Maji FC ya Songea katika uwanja wa Mkwakwani Tanga huku uwanja wa Sokoine Mbeya ukipigwa mchezo wa timu zote za jiji hiloTanzania Prisons dhidi ya Mbeya City.
Mechi ya Yanga na JKT Ruvu imemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-1, magoli ya Yanga yalifungwa na Donald Ngomadakika 33, Amissi Tambwe dakika ya 48 na 50 huku Thabani Kamusoko akipachika goli la nne dakika 87.
Matokeo ya mechi zingine zilizopigwa September 19
Stand United 2-0 African Sports
Mgambo Shooting 1-0 Maji Maji FC
Tanzania Prisons 1-0 Mbeya City
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin