Jumamosi ya September 26 ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania, kwani ndio siku ambayo tumepata nafasi ya kuona mechi ya kihistoria ya watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa uwanja waTaifa Dar Es Salaam.
Kabla ya kuchezwa kwa mechi hiyo ya kihistoria ambapo klabu ya Simba ndio ilikuwa timu mwenyeji wa mchezo huo, Simba na Yanga wamewahi kukutana mara 79, lakini klabu ya Dar es Salaam Young Africans kwa mujibu wa rekodi inaonekana kuwa mbabe kwa kuifunga Simba mara 29, huku Simba wakiwa wamewahi kuifunga Yanga mara 23 na kutoka sare mara 27. Hii ndio rekodi ambayo Simba na Yanga ziliingia uwanjani zikiwa zinaijua.
Mchezo umemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba, magoli ya Yanga yalifungwa naAmissi Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Malimi Busungu na kuandika goli la kwanza.
Goli la pili lilifungwa na Malimi Busungu kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa SimbaPeter Manyika na kuingia wavuni dakika ya 79. Mechi ilimalizika kwa Mbuyu Twitekupewa kadi nyekundu baada ya kuchelewesha muda ukizingatia alikuwa na kadi ya manjano.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa September 26
Coastal Union 0 – 0 Mwadui FC
Tanzania Prisons 1 – 0 Mgambo Shooting
JKT Ruvu 0 – 1 Stand United
Mtibwa Sugar 1 – 0 Maji Maji FC
Kagera Sugar 0 – 0 Toto Africans
Social Plugin