Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZIKO HAPA PICHA JINSI LOWASSA ALIVYOFANYA KUFURU NYUMBANI KWA DKT MAGUFULI..NI BALAA


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015. 





Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnaji Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato, Dkt. Benedicto Lukanima, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.





Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ameingia katika wa mkoa wa Geita kunadi sera za UKAWA na kupata mapokezi ya kishindoyawafuasi wa mabadiliko wakiwemo vijana ambao wamesema harakati zinazofanywa na CCM kumchafua Mh Lowasa hazina nafasi kwani watanzania wamechoshwa na ahadi zisizo na vitendo. 

Mh Lowassa ambaye ameanza kunadi sera za UKAWA katika wilaya ya Bukombe, Mbogwe alipofika katika jimbo la Chato anakotoka mgombea urais wa CCM Mh John Pombe Magufuli, alilakiwa na maelfu ya wananchi wanaounga mkono mabadiliko wakiwa na shauku kubwa ya kusikia UKAWA ilivyojipanga kuwaondolea matatizo yanayowakabili.

Alipowasili katika wilaya ya Geita ambayo inautajiri mkubwa wa dhahabu Mh Lowassa pia alikuta umati mkubwa ukimsubiri ulioanza kuingia eneo la mkutano sanne asubuhi, huku vijana wakipaza sauti zao za malalamiko ya uonevu wanaofanyiwa wanayodai kuwa ufumbuzi wake ukokwa Mh Edward Lowassa.

Mh Lowassa, viongozi na makada wengine wamewaambia wananchi hawa kuwa ufumbuzi wa matatizo yao ni jambo linalowezekana kinachohitajika ni kuitoa CCM madarakani na kuwachagua viongozi wa UKAWA ili waanze utekelezaji.

Mh Lowassa bado anaendelea na ziara ya kunadi sera za UKAWA katika kanda ya ziwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com