Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MKUTANO WA WADAU WA HABARI MKOANI SHINYANGA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU TANZANIA



Hapa ni katika ukumbi wa Katemi Hotel uliopo Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa wadau wa habari mkoani Shinyanga ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club-SPC) ikiwa ni agizo la Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania(UPTC) lengo likiwa ni kujadili namna wadau mbalimbali watakavyoshirikiana kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao wa rais,wabunge na madiwani unakuwa huru na wa haki.Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Uchaguzi huru na haki bila waandishi wa habari kuzingatia maadili ni ndoto.Mgeni rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga



Mgeni rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua mkutano huo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili yao ikiwa ni pamoja na kuepuka kupendelea mgombea wala chama siasa




Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga alipongeza pia kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika kuutangaza mkoa huo na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika mkoani humo



Mgeni rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliwataka waandishi wa habari kutoandika habari za kupotosha jamii lakini pia kuepuka kununuliwa.



Mgeni rasmi akiteta jambo na mwenyekiti wa Shinyanga Press Club



Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea



Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa taarifa kuhusu klabu hiyo ambayo sasa ina wanachama 38,kati yao 18 wanatoka wilaya ya Shinyanga,19 wilaya ya Kahama na mmoja kutoka wilaya ya Kishapu.Katika taarifa hiyo bwana Malunde aliwakumbusha wandishi wa habari kuzingatia maadili katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi na kuongeza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuhubiri amani kupitia kalamu zao.



Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde aliwataka waandishi wa habari kuepuka habari za uchochezi na kutojiingiza katika siasa na kushabikia vyama vya siasa



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika mkutano huo



Waandishi wa habari wakiwa ukumbini



Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini



Mkutano unaendelea



Katibu mtendaji wa Shinyanga Press Club akizungumza katika mkutano huo



Mkutano unaendelea



Mkutano unaendelea



Wadau wakiwa ukumbini


Endelea kuangalia matukio katika picha hapa chini



























































Picha zote na Emmanuel Mpanda,Stephen Wang'anyi,Patrick Mabula na John Mponeja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com