Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12 kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.
Nimekuwekea hapa chini Video 2 za Mchungaji Mtikila akizungumzia kuhusu Uchaguzi mkuu ujao lakini pia baada ya kukatwa na NEC kugombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Moja ya kauli yake ni Kuhusu afya ya mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa kwamba Ikulu siyo ICU...
Play pia Video Hii
Social Plugin