Gari aliyopata nayo ajali Mch.Christopher Mtikila
Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba mwenyekiti wa Chama cha DP nchini Tanzania mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia asubuhi hii Majira ya saa 12 kasorobo katika ajali katika Kijiji cha Msolwa karibu na mji wa Chalinze barabara ya Morogoro mkoani Pwani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jafari Ibrahim amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
"Kwa maelezo ya dereva,gari ndogo ,waliyokuwa wanasafiria iliacha njia wakiwa wanaelekea jijini Dar es salaam,ikapinduka,ilikuwa na watu wanne akiwemo dereva na mchungaji Mtikila,hawa watatu ni majeruhi na mchungaji Mtikila inasemekana amefariki,mwili wa marehemu na majeruhi wako njia wakielekea hospitali ya Tumbi",amesema Kamanda Ibrahim.
Social Plugin