VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika
kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine
21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni
Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Ni kweli jana majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana
wa JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21.
"Wengine wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma" alisema Dkt Fadhili.
Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.
"Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya
waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi
hawana fahamu"alisema.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema
chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na
kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.
Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani
ambapo lori hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa
limebeba makreti ya soda na unga.
Chanzo-Udakuspecially blog
Social Plugin