Hapa ni ndani ya Ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako leo Oktoba 09,2015 mchana,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga amemuapisha mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa anayechukua nafasi ya Benson Mpesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Kawawa ameanza rasmi kazi ya ukuu wa wilaya ya Kahama mara tu baada ya kumaliza kula kiapo cha kazi siku chache tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.soma>>HAPA
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mpya Hawa Ng'humbi anayechukua nafasi ya Wilson Nkhambaku ambaye amehamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha ataapishwa siku ya Jumatatu Oktoba 12,2015 baada ya kupata udhuru leo.
Zoezi la kumuapisha mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa Shinyanga pamoja na kuhudhuliwa na mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro watendaji wa mkoa na manispaa ya Shinyanga ikiwemo na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Marco Maduhu alikuwepo wakati mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akiapishwa leo,ametusogezea picha 14..Tazama hapa chini
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa (wa pili kulia) akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akisaini hati ya kiapo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisaini hati ya kiapo baada ya mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa kuisaini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akimkabidhi vifaa ya kazi mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa
Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akiwa ameshikilia vitendea kazi ikiwemo katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akivalishwa taji na mwanaye
Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akivalishwa taji na mkewe
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga na Familia ya mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa
Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Shinyanga,mkuu wa wilaya ya Kahama na familia yake
Picha ya pamoja viongozi wa mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa pia kuna mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(wa tatu kutoka kulia) aliyehudhuria zoei hilo
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Social Plugin