Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA ALIYESAMBAZA UJUMBE KUWA MKUU WA MAJESHI AMELISHWA SUMU AFIKISHWA MAHAKAMANI




Kijana aliyetuma taarifa katika mtandao wa facebook kuwa mkuu wa jeshi la wananchi Jenelali Davis Mwamunyange amewekewa sumu amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kutoa taarifa za uwongo ambazo zililenga kuupotosha umma.

Mbali na kijana huyo Benedikiti Ngonyani pia walipandishwa kizimbani raia wengine kutoka Pakistani, China na Afrika ya Kusini wakikabiliwa na mashtaka ya kuingilia njia za mawasiliano bila ya kibali kutoka katika mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA na kusababisha serikali kukosa kodi.

Washtakiwa hao wote walikuwa wanasomea mashtaka yao mbele ya hakimu mwandamizi Respicius Mwijage ambapo katika shauri la kijana aliyetoa taarifa za uwongo kuhusu Mwamunyange ameendelwea kubaki rumande kutokana na mkurugenzi wa mashtaka kuweka pingamizi la dhamanana kutokana na sabua za kiusalama.

Katika shauri linaowahusu raia hao wa nje nao wameendelea kubaki ndani kutokana na mahakama hiyo ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo hadi mahakama kuu watuhumiwa wote sauri lao litaletwa tena Oktoba 23.

Wakizungumza na waandishia wa habari wakili mkuu wa serikali Johanes Karugura amesema kijana huyo alikamatwa Septemba 5 kwa kosa kwa kusambaza taarifa kuhusu mkuu wa majeshi.

Naye kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Charles Kenyela amewataka watu kuwa makini na kusambaza taarifa za uwongo kwani jeshi la polisi haliwezi kukaa kimya.

Kwa uapande wake mhandishi wa TCRA Sadata Karoli amesema raia hao wa nje wamesasabisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja kutokana na hujuma yao ya kuingi mifumo ya mawasilni ya mamlaka ya TCRA.


Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com