Jiji la kitalii la Arusha limesimama kwa muda kupisha mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa ukiongozwa na mgombea wa nafasi ya urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa.
Kwa wakazi wa jiji hili la kitalii na viunga vyake vyote la Arusha wanasema hizi ni salamu tu kuelekea Oct 25 mwaka huu.
Mkutano huu unaotajwa kuvunja rekodi ya mikutano ya hadhara jijini Arusha ulichagizwa na uwepo aliyekuwa kada namba 8 wa CCM, comledy Kingunge Ngombale Mwiru ambaye kwa sasa yuko na timu ya mabadiliko baada ya kukikacha chama chake cha zamani cha CCM.
Kwa upande wake waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye kwa maneno machache kabisa amesema kwa hali ilivyo nchini kazi imebaki moja ya kuhakikisha viongozi wa UKAWA wakiongozwa na Edward Lowasaa wanaongoza serikali ya wamu ya tano.
Akihutubia maelfu ya wakazi hao ambao licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha walikuwa wakiendelea kumsikiliza mgombea wa urais Edward Lowassa, amesisitiza kutumia speed 120 katika kuhakikisha mtanzania ananufaika na rasilimali za nchi.
Edwin Mtei masisi wa Chadema anasema ni wakati muafaka wa kukiongoa chama cha CCM kwani ndani ya miaka 54 ya uwepo wake kimedhihidilisha kushindwa kuwaongoza watanzania.
Mgombea huyo wa urais Edward Lowasa anayetajwa kuwa na mvuto zaidi katika kipindi hiki amefanya mikutano kadhaa kabla ya kuhitimisha kwa kishindo katika uwanja wa sinoni mjini arusha.
Edward Ngoyai Lowassa na Godbless Lema wakiwasili katika viwanja vya Sinoni Unga Ltd leo Alhamisi 8/10/2015
Social Plugin