Majira ya saa nane mchana alikuwa kwenye jukwaa la kampeni mjini Moshi.
Awali majira ya saa tano asubuhi aliwasili Tarakea mjini Rombo.
Edward Lowassa anayetamba kama mkombozi wa Tanzania ijayo, amesema kama watanzania watampa ridhaa ya kuwa rais atahakikisha anadhibiti vifo vya mama na mtoto hapa nchini.
Akiwa mjini Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya akatumia jukwaa hilo kutangaza neema kwa watanzania waishio mipakani
Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema taifa anasema nafasi hii ni muhimu kwa watanzania kuitumia kwa kukiondosha madarakani chama cha CCM kwani licha ya kushindwa kuleta mabadiliko bali pia kimechoka na hakipaswi kuendelea kuwepo madarakani.
Akiwa mjini Kilimanjaro Edwrad Lowassa usafiri wa chopa ulimrahisishia kazi kwa kufanya mikutano katika majimbo ya Rombo, Moshi mjini, Siha na Karatu ambapo comledy Kingunge Ng’ombale Mwiru akatoa neno kwa watanzania.
Social Plugin