MGOMBEA URAIS WA CHAUMMA HASHIM RUNGWE AFUNGUKA KUHUSU RASILIMALI ZA TANZANIA






Mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ukombozi wa umma (CHAUMA) Hashim Rungwe amesema akipewa ridhaa na watanzania ya kuingia ikulu atahakikisha kuwa anasimamia raslimali zilizopo nchini kwa ajili ya kuwasaidia watazania kwa sababu viongozi waliopo madarakani wameshindwa kutumia fursa hizo kuwakomboa watanzania na janga la umasikini.


Aidha mgombea huyo amesema endapo atapata ridhaa hiyo atashugulikia sula la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi kwa sababu nchi mbalimbali za Afrikia Mashariki ikiwemo Uganda wamafanikiwa na hivi sasa wanatakeleza majukumu yake bila kuwa na machafuko kama jinsi inavyoripotiwa na ikianzishwa nchini kutakuwa na machafuko.

Kwa upande wake mgombea mwenza kwa tiketi ya chama hicho Issa Hussein amewataka wananchi kubadilika katika zoezi la upigaji kura katikia uchaguzi mkuu ujao kwa sababu wakati umefika kwa wananchi kuhoji maendeleo kwa chama cha CCM kilichotawala kwa miaka 50 lakini bado asilimia kubwa ya watanzania wanazidi kudhoofika kiuchumi.

Kufuatia hatua baadhi ya wananchi wa jiji la Tanga wamewashauri wakazi wa mkoa wa Tanga na nchi nzima kwa ujumla kuchagua viongozi ambao wana sera zenye kugusa maisha ya watanzania badala ya kushabikia vyama.

Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post