KUHUSU MGOMBEA URAIS WA TLP KUZUIWA KUPIGA KURA..




Mgombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo ameshindwa kutekeleza haki yake ya msngi na ya kikatiba ya kupiga kura leo baada ya kukosekana kwa fomu namba 19 inayo mruhusu kupiga kura kwa kuwa hayupo kituo chake cha kupigia kura cha Dar es Salaam alichojiandikisha awali ambapo kwa sasa yupo jijini Arusha.

Mbali na kukosekana kwa fomu hiyo, Mgombea huyo pia hakuwa na kitambulisho chake cha kupigia kura.

Hata hivyo Habari tulizozipata baadaye ni kwamba Mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo amepiga kura yake muda mfupi uliopita, amesema hapakuwa na fomu namba 19 lakini kitambulisho alikuwa nacho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post