Msemaji wa chama ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya, alisema wataendeleza na kuyaenzi yote aliyoyaacha marehemu kwa manufaa ya chama chao na taifa.
Alisema watahakikisha wanaenzi Utanganyika pamoja na kufichua maovu pamoja na kuwa watetezi wa Watanzania.
“Tunatarajia kuendelea pale alipoishia Mwenyekiti wetu kuhakikisha tunayaenzi aliyoyaacha na kufuata nyayo zake ikiwa ni pamoja na kuuenzi Utanganyika,” alisema Mluya.
Anayekaimu nafasi ya Mtikila ni Makamu Mwenyekiti wa DP Zanzibar, Peter Mapwila, alisema wanatarajia kuendeleza kesi zote alizozianzisha katika mahakama mbalimbali nchini.
Alisema mfano wa kesi mbili ambazo wanazifanyia kazi ni ya Mchungaji Mtikila kuzuiwa kuwania nafasi ya urais pamoja na ile aliyomfungulia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, kufanya kampeni kabla na wakati akiwa CCM.
Chanzo-Eddy blog
Social Plugin