Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru. Kingunge amezungumza leo mbele ya waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam.
Amesema kutokana na matukio yaliyotokea katika kumpata mgombea Urais kupitia chama chake ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo ameamua kuondoka ndani ya chama hicho na sasa yupo huru.
Kingunge amesema hawezi kuhimili chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee na makada wengine.
Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki zake za kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi yake..”Hali ya sasa jinsi ninavyoona vijana, wafanyakazi, wakulima wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa mabadiliko kwa sababu wakati tukiwa TANU tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”…KINGUNGE.
Kingunge- "Kila unapopita vijana,kinamama, na watanzania wote wanataka mabadiliko na mimi niko upande wa mabadiliko na yaje haraka"
Kingunge- "Wanabadilisha kibwagizwo toka kidumu 'chama cha mapinduzi' hadi 'kidumu chama tawala', hapo ni kung'ang'ania madaraka"
Kingunge- "Baada ya kukaa madarakani muda mrefu chama cha CCM hakiwezi kufanya jipya, chama kikikaa nusu karne hakina jipya tena"
Kingunge- "Mabadiliko ni muhimu kweli kweli, upate watu wengine wenye pumzi mpya, mnataka mbakie nyinyi tu, nyie pumzi imekwisha"
Kingunge -" Sisemi chama hiki cha zamani kisifanye kazi, kiwekwe kando kwa muda, CCM imeacha kujadili issues sijui wanajadili nini"
Kingunge- "Wanaotaka tuondoke hapa twende mbele lazima watu wapya waongoze, lazima fikra mpya ziongoze".
Kingunge- "Tumefika mahali pagumu sana, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa ila kwa utafiti wangu nguvu ya wanaotaka mabadiliko ni kubwa zaidi hivyo msiogope" amemalizia kwa kusema hayo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin