Oktoba 03,2015 waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kupitia klabu ya waandishi wa habari mkoani humo(Shinyanga Press Club) wamepatiwa mafunzo maalumu juu ya mpango wa KIKOA-Bima ya afya kwa wajasiriamali kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (National Health Insurance Fund).
Mkutano huo uliolenga kutoa elimu kuhusu mpango wa Kikoa(Bima ya afya kwa wajasiriamali katika vikundi) ,umefanyika katika Ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga na mgeni rasmi alikuwa ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe.
Kwa mujibu wa NHIF Mpango wa Kikoa ni utaratibu wa utoaji wa huduma za afya kwa kadi kwa vikundi/ushirika vilivyo katika sekta isiyo rasmi mfano VIBINDO,SACCOS,AMCOS,VIKOBA na vikundi maalum vya wajasiriamali vilivyosajiliwa na sasa Klabu za waandishi wa habari-Picha zote na Paul Kayanda- Malunde1 blog
Mkutano huo uliolenga kutoa elimu kuhusu mpango wa Kikoa(Bima ya afya kwa wajasiriamali katika vikundi) ,umefanyika katika Ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga na mgeni rasmi alikuwa ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe.
Kwa mujibu wa NHIF Mpango wa Kikoa ni utaratibu wa utoaji wa huduma za afya kwa kadi kwa vikundi/ushirika vilivyo katika sekta isiyo rasmi mfano VIBINDO,SACCOS,AMCOS,VIKOBA na vikundi maalum vya wajasiriamali vilivyosajiliwa na sasa Klabu za waandishi wa habari-Picha zote na Paul Kayanda- Malunde1 blog
Aliyesimama ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkurugenzi wa mtandao huu wa Malunde1 blog, ndugu Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano huo
Aliyesimama ni meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Amani Immanuel akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo alisema mpango wa Kikoa ni mpango mpya ulioanzishwa mahsusi kukidhi haja ya kundi la watu wa kati ambao hawawezi kujilipia bima kama watu binafsi na hawaridhiki kujiingiza katika mfumo wa CHF kwa ukomo wa faida katika mfuko wa Kikoa.Kulia kwake ni Afisa Udhibiti wa ubora NHIF mkoa wa Shinyanga na Simiyu Dr Gustav Kisamo
Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Suzy Butondo akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini ambapo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga walisisitizwa kuwa wanachama wa NHIF kupitia utaratibu wa KIKOA kwa ajili ya kuwa na uhakika wa afya zao kwani hakuna anayejua ataugua lini,wakati huo huo hujui kama siku ukiugua utakuwa na pesa ya kufanikisha matibabu au la.
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Amani Immanuel akizungumzia faida za kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya kwa waandishi wa habari ambazo ni pamoja na kupata matibabu mahali popote nchini,kuepuka kuomba msaada pindi unapougua kwani unakuwa umejiwekea akiba na faida nyingine nyingi.Meneja huyo wa NHIF alisema mwanachamawa NHIF katika utaratibu wa KIKOA atapata mafao yote yanayotolewa na NHIF sawa sawa na wanachama wengine wa NHIF wanaojiunga kwa taratibu nyingine
Mgeni rasmi Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kujiunga na mfumo wa taifa wa bima ya afya kwani una faida kubwa na ikumbukwe kuwa siyo wakati wote binadamu anakuwa na pesa,hivyo kupitia mfuko huo hata kama hatakuwa na pesa atapata matibabu bila gharama yoyote.Aliongeza kuwa taifa linahitaji watu wenye afya hivyo ni vyema kila mwananchi akaona umuhimu wa kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa afya yake
Mkutano unaendelea
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe alitoa wito kwa wananchi kujiunga na NHIF kwani matibabu kwa njia ya kadi yanapunguza pia mianya ya rushwa katika maeneo ya matibabu
Afisa Uanachama NHIF mkoa wa Shinyanga Mohamed Katoto akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema mwanachama wa NHIF atachangia shilingi 76,800/= kwa mwaka na atapatiwa kadi ya matibabu ya NHIF aatakayoitumia kupata matibabu katika vituo zaidi ya 6000 vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima
Afisa Uanachama NHIF mkoa wa Shinyanga Mohamed Katoto akiwasisitiza waandishi wa habari kujiunga KIKOA,kulia ni mwandishi wa habari ITV/Radio One bwana Frank Mshana.Katoto alisema mwanachama wa KIKOA ana nafasi ya kuwaingiza mwenza wake na nafasi nne kwa ajili ya watoto(miaka 18 au 21 kama bado anasoma) na wazazi wake na wa mwenza wake kwa utaratibu wa kuwachangia kila mmoja wao kiwango hicho cha shilingi 76,800 kwa mwaka.
Makamu mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Shaaban Alley akiuliza swali wakati wa mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo ndugu Chibura Makorongo akizungumza wakati wa mkutano huo
Afisa Udhibiti wa ubora NHIF mkoa wa Shinyanga na Simiyu Dr Gustav Kisamo akizungumzia kuhusu mafao ambayo mwanachama wa KIKOA atapata.Alisema mafao hayo ni pamoja na Ada ya kujiandikisha na gharama za kumwona daktari,huduma ya wagonjwa wa nje,huduma ya wagonjwa wa ndani,gharama ya vipimo na dawa,upasuaji,tiba ya kinywa na meno,tiba ya macho na miwani ya kusomea,vifaa saidizi mfano vya kusaidia kusikia,mikanda ya mgongo n.k
Afisa Matekelezo NHIF mkoa wa Shinyanga bi Neema akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Picha ya pamoja maafisa kutoka NHIF na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga baada ya mkutano kumalizika
Picha ya kumbukumbu
Picha zote na Paul Kayanda- Malunde1 blog
Social Plugin