Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YALALAMIKIWA KUTELEKEZA WAZEE WASIOJIWEZA




Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya wazee duniani baadhi ya wazee, wasiojiweza, walemavu wa viungo na walemavu wa ngozi Albino wameshangazwa na serikali kwa kuwatelekeza miaka mitatu bila huduma za chakula na dawa za matibabu na kuwafanya waishi kwa kutegemea misaada ya wasamalia wema wakati wizara ya afya na usitawi wa jamii inapata ruzuku ya seikali kila mwaka hali inayohatalisha maisha ya watu. 


Wazee hao wanaoishi makao ya wazee na wasiojiweza kituo cha Bukumbi wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza akiwemo bibi mwenye umri unaokadiliwa kuwa na miaka 90 amepofuka, kiziwi, amepooza miguu kutokana na tatio la moyo na wengine hawana uwezo wa kutembea wanalazimika kujiburuza chini kwa kukosa msaada unaositahili.

kufuatia hali hiyo taasisi inayojihusisha kuboresha huduma za afya vijijini iliyoanzishwa na madakitali wazalendo wa kitanzania wakishirikiana na kampuni ya ako kwa lengo la kuhudumia makundi maalumu yasiyojiweza timu ya wataaramu ikafika makao ya wazee na wasiojiweza Bukumbi wakiwa wamesheheni chakula na dawa ambapo wametoa msaada wa matibabu bure kwa wagonjwa.

Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo afisa mfawidhi makao ya wazee na wasiojiweza Bukumbi Bw.Marco Bundala amekili kushindwa kuwahudumia wazee kutokana na bajeti ndogo inayotolewa na serikali ambayo haitoshelezi mahitaji ya chakula na dawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com