Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAARIFA ZAIDI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA...ALIPANDA GARI LA KUKODI


Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia katika ajali ya gari dogo walilolikodi wakitokea Njombe katika mkutano wa kampeni wa chama chake wakirejea jijini Dar es Salaam na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka eneo la Msolwa Chalinze Bagamoyo mkoani Pwani.


Majeruhi wawili walionusirka katika ajali hiyo akiwemo mchungaji Patrick Mgaya ameelezea namna ajali hiyo ilivyotokea akisema chanzo ni mwendo kasi wa dereva wa gari walilokuwa wamekodisha licha ya marehemu mchungaji Mtikila kumsihi apunguze mwendo mara kwa mara huku Bw. Ali Mohamed aliyelazwa katika hospitali teule ya rufaa Tumbi Kibaha akishindwa kuelezea kutokana na maumivu makali ya mwili aliyoyapata katika ajali hiyo.

Tumetoka Njombe tukiwa salama,tulipofika Morogoro kuweka mafuta...mchungaji hakuwa amefunga mkanda...tulipofika Msolwa tukapishana na lori likiwa katika mwendo kasi...akaamua kuondoa gari barabarani"amesema

Mdogo wa marehemu Bw.Charles Ben Mtikila amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo amesema wakati wa uhai wake marehemu hakuwahi kumuaga safari yake ya Njombe na taarifa alizipata baada ya kupigiwa simu na msamaria kutoka mkoani Musoma huku wananchi wanaomfahamu mchungaji Mtikila wakielezea masikitiko yao juu ya kifo hicho.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani kamanda Jaffari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kushikiliwa kwa dereva wa gari dogo lenye namba za usajili T189 AGM Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na dereva George Steven Ponela ambapo Dk kiongozi wa hospitali teule ya Tumbi Kibaha Dk Peter Dattan amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi na mwili wa marehemu mchungaji Mtikila umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

SOMA ZAIDI NA ANGALIA PICHA HAPA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com