Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia!! MGOMBEA UBUNGE ARUSHA MJINI AFARIKI DUNIA


Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Estomih Malla amefariki dunia katika hospitali ya KCMC Moshi.
Akizungumza na Malunde1 blog hivi punde Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ameithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki dunia kutokana na kuumwa kichwa sana.

Hata hivyo habari zinasema kuwa  Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu na kusababisha kifo chake usiku wa Oktoba 9, 2015 saa saba usiku.

Inaelezwa kuwa hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadaye kukimbizwa hospitali ya St Thomas.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hospitalini hapo kutoka kwa madaktari ni kwamba Malla alikuwa anasumbuliwa na uchovu na hivyo alitakiwa kupumzika kwa muda mrefu. 

Afisa Habari wa ACT Wazalendo Abdallah Hamis mesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Malla.Amina!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com