Vyama vya siasa vya TLP na CCM vimewataka viongozi wa vyama vya umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wawaombe radhi watanzania kwa unafiki waliounyesha awali wa kumkashifu mh edward lowasa kuwa ni fisadi na sasa wanamtakasa kuwa ni mtu safi anayefaa kuliongota taifa.
Mwenyekiti wa taifa wa TLP Dr.Augustine Mrema na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya hai Bw.Amani Uronu wametoa rai hiyo kwa nyakati tofauti walipoongea na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro juu ya mchakato wa uchaguzi unaoendelea nchini.
Dr.Mrema na Bw.Uronu wamesema,kitendo cha viongozi hao kinaua upinzani ndani ya nchi na kuwafanya wapinzani wasieminike kwa kuwa vigeugeu ndani ya jamii.
Kauli hiyo imeungwa mkono na mchungaji Joachim Mmanyi wa kanisa la Pentekoste na kwamba viongozi hao wametenda dhambi ya unafiki dhidi ya Dr.Wilboard Slaa aliyetarajiwa wananchi wampigie kura ya urais na badala yake kumweka mtu aliyetuhumiwa kwa ufisadi.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango wakiwasalimu wakazi wa Same waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za
CCM Ndungu.PICHA NA MICHUZI JR-KILIMANJARO.
Wakazi wa Same Mashariki wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimvalisha fulana mmoja wa wafuasi wa CHADEMA alieamua kurejea chama cha CCM jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya jimbo la Same Mashariki
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ndungu kweye mkutano wa kampeni Same Mashariki,jioni ya leo.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo,Innocent Shirima wakiwapungia wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni mjini himo.
Wakazi wa Himo wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Vunjo kupitia CCM Innocent Shirima.
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Mwanga.
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Same Magharibi kwenye uwanja wa Kwasakwasa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa katika uongozi wake atahakikisha kodi ndogo ndogo zinaondolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
Wakazi wa Same Magharibi wakishangilia mara baada ya kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uwanja wa Kwasakwasa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa katika uongozi wake atahakikisha kodi ndogo ndogo zinaondolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
Mgombeawa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema mara baada ya kukutana njia panda ya
Himo.
Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema akizungumza mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM na kuwataka wananchi wa Vunjo kumpigia kura mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli
kwani ni rafiki wa kweli kwa maendeleo ya Tanzania.
Social Plugin