TUME YA UCHAGUZI YAFUNGUKA KUHUSU WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU UJAO TANZANIA
Wednesday, October 07, 2015
Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 leo Octoba 7, 2015 Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva ametolea majibu kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi mkuu.
‘Suala la Wanafunzi mara kwa mara limekuwa likiletwa na sisi kwenye tume tumesema kwamba linafanywa kama la kisiasa kwa maana kwamba mara kadhaa wanafunzi walipokuja pale ofisi za tume kile kikundi chao wakatuambia kwamba kipindi hiki watakuwa likizo‘ Lubuva
‘Tukawapa ushauri na tukazungumza nao nimeenda mpaka chuo cha Dodoma tukazungumza nao na tukawapa utaratibu mpaka tukaunda kamati ikaongozwa na Jaji Mkwawa wasikilizwe wakaelezwa na baadae wakaandikiwa barua kwa hiyo hili suala ni suala la kisiasa na tumeshughulika nalo mwisho tukawaambia kwamba wamejinyima wenyewe hii nafasi’- Lubuva
‘Kwa hiyo suala la wanafunzi ninasema kwa niaba ya wenzangu kwamba kwenye tume tumefunga mlango na upande wa kuboresha daftari umepita ni wao wenyewe wamejinyima na kuhusu kwamba vyuo vifungwe kwasababu ya Uchaguzi Mkuu ni suala la Wizara ya Elimu sio la tume ya Uchaguzi – Lubuva
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Jaji Damian Lubuva
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin