Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UMEZIONA PICHA ZA MAFURIKO YA LOWASSA LEO JIJINI DAR ES SALAAM? ZIKO HAPA


Mgombe Urais wa CHADEMA Mhe. Edward Lowassa akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Saed Kubenea


Msafara wa Mgombea Urais wa CHADEMA akiwa maeneo wa Ubungo akiendelea na kampeni.. Jijini Dar es Salaam.

Wakazi wa Mwembeyanga, Temeke waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa CHADEMA Mhe. Edward Lowassa.




Mgombe Urais wa UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke.


Makongoro Mahanga akimnadi Julius Mtatiro wa Jimbo la Segerea kupitia CUF na UKAWA.

Wakazi na wafanya biashara wa eneo na Ubungo wamemsimamisha Mgombea Urais wa CHADEMA, Mhe Edward Lowassa kuongea nae








TANGANYIKAPACKERS: Wananchi wakimsubiri Edwardlowassa kwa ajili ya mkutano wa kampeni













Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Bwana Edward Lowassa amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ya Oktoba 25 kupiga kura na kuzilinda ili kuwezesha umoja wa katiba ya wananchi kuingia madarakani.


Akizungumza katika mkutano minee ya kampeni akianzia katika viwanja vya Mwembeyanga, Mhe. Lowassa licha ya kufurahishwa na idadi ya watu waliofika viwanjani hapo na kuahidi kumpigia kura za ndio ameelezea sababu ya kugombea uraisi na kuahidi akiingia madarakani atafanyakazi ya kazi ya kuwaletea maendeleo kwa kasi kubwa.



Waziri mkuu mstaafu Bwana Fredrick Sumaye ametaka wakazi wa Dar es Salaam kumpigia kura ya ndio mgombea urais Bwana Edward Lowaasa ili aweze kuingia madarakani ili aweze kurejesha sifa na maendeleo ya Tanzania pamoja na kuwaondoa watanzania katika lindi la umasikini.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa kampeni uliofanyika Sinza Lowassa amewataka wakazi wa eneo hilo na maene ya jirani kuhakikisha wanampa kura za kutosha.



Aidha, Bwana Lowassa ametumia mikutano hiyo kuwanadi wagombea ubunge katika jimbo la Temeke, Kawe na Ubungo kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, ambapo wagombea walipata fursa ya kueleaza kero na matatizo katika maeneo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com