Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU WANNE WAFUNIKWA NA KIFUSI MACHIMBO YA DHAHABU NYANGALATA KAHAMA


Watu wanne wanahofiwa kufukiwa na kifusi katika maachimbo madogo ya Dhahabu ya Nyangalata Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga huku wengine 11 wakiokolewa na kulazwa katika kituo cha afya Lunguya wilayani humo.



Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea juzi katika Mashimo manne yaliokuwa na Wachimbaji zaidi 20.

Amefafanua kuwa tukio hilo limetokea mfululizo kwa siku moja ambapo tukio la kwanza lilitokea majira ya saa tatu asubuhi huku la pili likitokea majira sita mchana.

Kamugisha amesema inahofiwa kuwa wachimbaji hao Wanne bado wamo ndani ya mashimo hayo, kwani pindi wenzao wanapofanya mawasiliano nao kwa njia ya simu za mkononi, simu zao zimekuwa zikiita.


Kwa upande wake Diwani aliyemaliza muda wake katika kata ya Lunguya yaliyopo machimbo hayo Benedicto Manwari amesema kulikuwa na Duara nne zilizoanguka na kujeruhi watu 11 ambao wanaendelea kupata matibabu katika kituo cha afya Lunguya.

Amesema kuwa sasa Jitihada zinafanyika za kuwaokoa Wachimbaji wengine ambao inasadikiwa wapo ndani ya mashimo kwa kushirikina na kikosi cha uokoaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu.

Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu tukio hilo, Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama Sophia Omary amesema hawezi kuzungumzia kwani yupo safarini kuelekeaa eneo la tukio na kuahidi kutoa ufafanuzi pindi atakapojiridhisha na hali ya eneo hilo.

Chanzo-Dunia Kiganjani Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com