Novemba 12,2015 Kijana Richard Ndariro maarufu kwa jina la BOB RICH ama RND,ambaye ni mtangazaji maarufu wa Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga ambaye huendesha vipindi mbalimbali kikiwemo kipindi cha Faraja Mamboleo na Michapo ya Jioni anatangaza rasmi kuachana na radio hiyo na kuendelea na shughuli zingine tofauti na utangazaji....Usiku huu imefanyika hafla fupi na ya kushtukiza iliyohudhuriwa na baadhi ya watangazaji wenzake,marafiki na baadhi ya wapendwa wake katika eneo la bwalo la Jeshi Kambarage mjini Shinyanga...Pichani ni keki iliyoandaliwa kwa ajili yake...Nimekuletea picha 37 kilichojiri....Tazama hapa chini
MC wa Hafla fupi na kushtukiza kumuaga Richard Ndariro,,,bwana Faustine Kasala ambaye ni mtangazaji wa Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi
Watangazaji wa radio Faraja na wageni waalikwa
Kulia ni mtuma salamu maarufu nchini Tanzania anajulikana kwa jina la Mr Timberland/Gavana wa Shytown akifuatiwa na Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stephen Wang'anyi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi ya kumuaga Richard Ndariro(wa pili kutoka kushoto),anayefuatia ni Agnes Kambarage kutoka Radio Faraja
Kushoto ni mtangazaji wa Radio Faraja Veronica Natalis maarufu kwa jina la V2 ambaye anawakilisha radio DW
Mkurugenzi wa Mipancho Entertainment bwana Egam Dropper akiwa eneo la tukio
Kushoto ni mtangazaji wa Radio Faraja bwana Faustine Kasala
Keki
Richard Ndariro akikata keki
Zoezi la kukata keki linaendelea
Bob Rich akimlisha keki mgeni rasmi Bwana Stephen Wang'anyi
Bob Rich akimlisha keki mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja bwana Anikazi Kumbemba
Bob Rich akimlisha keki Egam Dropper
Bob Rich akimlisha keki Faustine Kasala
Bob Rich akikumbatiana na mjukuu wake baada ya kumlisha keki
Bob Rich akimlisha keki Mtangazaji wa Radio Faraja Steve Kanyefu maarufu kwa jina la Mwanaporii
BOB RICH akilishwa keki
Mtuma salamu maarufu nchini Tanzania Mr Phone aka mzee wa Check akizungumza alivyomfahamu Bob Rich
Veronica Natalis akieleza jinsi BOB Rich alivyokuwa msaada Radio Faraja kwamba alikuwa mtu wa kujituma anayependa kazi na mbunifu katika vipindi mbalimbali vya radio
Hafla inaendelea
Mwanaporii..mtangazaji wa Radio Faraja akisimulia jinsi BOB Rich alivyokuwa anajituma katika kazi na kushauri pia kusaidia wengine
Veronica Natalis akimlilia BOB Rich
Bob Rich akiangalia zawadi zake
Mkurugenzi wa Mipancho Entertainment Egam Dropper aliyewakilisha wasanii wa Shinyanga akizungumza katika hafla hiyo fupi
Egam Dropper akisimulia jinsi Bob Rich alivyokuwa mwepesi wa kuchukua na kucheza radioni nyimbo za wasanii wa Shinyanga
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari pia mkurugenzi wa Malunde1 blog bwana Kadama Malunde,ambaye amewahi kuwa mwandishi wa habari,Mtangazaji na Mhariri mkuu wa habari wa Radio Faraja akizungumza katika hafla hiyo ambapo alieleza jinsi BOB Rich alivyokuwa anajituma katika kazi na ubunifu wake katika kazi ya utangazaji
Mr Timberland/Gavana wa Shytown akisimulia jinsi Bob Rich alivyokuwa anathamini watuma salamu kwa njia ya Radio katika vipindi vyake
Veronica,Eliza na Agnes kutoka Radio Faraja wakiwa katika hafla hiyo
Mkurugenzi msaidizi wa radio Faraja Anikazi Kumbemba akizungumza katika halfa hiyo fupi na ya kushtukiza ambapo aliwataka watangazaji wengine kuiga mfano wa Bob Rich kwani ni kijana anayejituma,mwadilifu,mvumilifu na mbunifu
Mgeni rasmi Stephen Wang'anyi akizungumza katika hafla hiyo fupi na ya kushtukiza
Bob Rich akiwashukuru wafanya kazi wa Radio Faraja,wadau na marafiki zake na kudai kuwa sasa anaachana na kazi ya utangazaji na ataendelea na kazi nyingine tofauti na ya uandishi wa habari
Chakula cha pamoja nacho kilikuwepo....
Zoezi la kuchukua chakula likaendelea
Kila mshiriki alikula na kunywa
Tunakula pamoja baada ya kumuaga BOB Rich
Tunakula....
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog