BAADA YA KUUKACHA USPIKA!! MHESHIMIWA ANNE MAKINDA AMTAKA SPIKA AJAYE ASIWE NA HASIRA...




Spika wa bunge anayemaliza muda wake Mh Anne Makinda amemtaka spika ajaye kutokuwa na hasira na badala yake awe mtulivu kwa kujifunza aina ya wabunge alionao na tabia zao ndipo ataweza kuendesha vikao bila mikwaruzo.


Mh Makinda Ametoa wito huo jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatagombea tena nafasi hiyo baada ya kukaa bungeni kwa kipindi cha miaka 40 .

"Mheshimiwa Kikwete ni rika yangu amestaafu, ninaona ni wakati wangu na mimi nipumzike na kuwapisha wengine..Ukifika miaka 40 ya uongozi ni vizuri ukaona na wengine wanataka kufanya nini, ukiangalia rika yangu wengi wamestaafu",alisema Makinda.




"Nitawamis sana, wengine walisema napendelea lakini sikuwa napendelea chama chochote wengine walikuwa watundu na saa nyingine unaamua kumuweka yule Mbunge mtundu kabisa ili achangamshe bunge,Ukipata wabunge wachangamfu kama waliopita hata kanuni unazijua tu,huwezi kusahau, lilikuwa Bunge zuri sana",aliongeza

 Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo mengine.


Awali mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.

“Mimi ndugu yako kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa ko kama mbunge wangu, naomba kugombea uspika kwa mara nyingine, kwa msaada w Mwenyezi Mungu nakutegemea sana naomba uniunge mkono. Asante kwa ukarimu wako,” ilisomeka sehemu ya ujumbe unaoaminika kuwa ulitumwa na Anna Makinda kwa wabunge wateule.

Hata hivyo, hadi pazia la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafungwa, Mama Anna Makinda alikuwa hajarudisha fomu yake hivyo kuonesha dhahiri kuwa ameachana na mpango huo.


Makada wengi wa CCM wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.Dkt. Emmanuel Nchimbi, Samwel Sitta, Dkt Didas Masaburi, Balozi Philip Marmo, Mussa Hassan ‘Zungu’, Job Ndugai, Abdallah Mwinyi ni miongoni mwa majina ya makada wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.


Katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam zoezi la makada wa chama hicho kuchukuwa fomu za kugombea uspika na unaibu spika limeendelea ambapo wamefikia wagombea 23 ambapo wagombea 22 wanagombea uspika na mmoja unaibu spika.

Via>>ITV,EATV na Udakuspecially.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post