RAIS MAGUFULI AMTEUA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU,ATHIBITISHWA KWA KURA 258 ZA NDIO
الخميس, نوفمبر 19, 2015
Hatimaye Kile kitendawili cha Nani Atakuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tano Kimepata jibu leo asubuhi.
Rais John Pombe Magufuli amemteua Mh Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina hilo limetangazwa leo na Spika wa bunge Mh. Job Ndugai.
Tayari Mh. Kassim Majaliwa amethibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu mteule kwa kupata kura za ndio 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote 351 zilizopigwa.
Kura za hapana ni kura 91 sawa na asimilia 25.9 ya kura zote, na kura zilizoharibika ni 2.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin