Dkt Tulia Mwansasu kutoka chama cha mapinduzi amechaguliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushinda kwa kura 250 kati ya kura 351 zilizopigwa na wabunge kutoka vyama mbalimbali ikiwemo chama tawala na vyama vya upinzani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nje ya ukumbi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuapa, Mh Dakta Tulia Mwansasu amesema atatumia taaluma yake ya sheria kusaidiana na Mh spika Job Ndugai kutekeleza majukumu yao bila kuegemea chama chochote huku mpinzani wake Mh Magdalena Sakaya kutoka chama cha wananchi CUF akikubali matokeo na kumpongeza dacta Tulia kwa ushindi huo.
Social Plugin