Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Duh!! UMEIPATA HII YA MBUNGE KUFUMANIWA NA MCHEPUKO HUKO DODOMA?? NI HATARI KICHAPO CHA HATARI KIMETEMBEA


IMESHANGAZA! Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama kimoja cha siasa chenye nguvu nchini ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa, yupo katika figisufigisu ya ndoa yake kuvunjika kufuatia kufumaniwa na mumewe...endelea na stori hapa chini


Tukio hilo la aibu lilijiri Alhamisi iliyopita kwenye hoteli moja mjini Dodoma ambapo mbunge huyo na mumewe walipiga kambi kwa ajili ya zoezi la wabunge kuapishwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mbunge huyo aliwasili mjini Dodoma na mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara, kwa lengo la kumpa kampani wakati akiapa kiapo cha utii kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

SIKIA SIMULIZI YAKE
“Ilikuwa Alhamisi iliyopita (Novemba 19, 2015), mheshimiwa huyo ambaye amepigana kusaka ubunge kwa miaka mingi bila mafanikio, alikwenda Dodoma na mume wake. Unajua tena, mama anaapishwa lazima baba uwepo.

“Kweli, mama aliapishwa vizuri, akawa mheshimiwa kamili. Shughuli hiyo ilipomalizika, walirudi kwenye ile hoteli waliyofikia,” kilisema chanzo hicho.

RATIBA YA MUME ILICHANGIA
“Sasa kumbe ratiba ilionesha kuwa, baada ya kuapishwa mama na kurudi hotelini, mista asingelala Dodoma. Ilikuwa lazima arudi kwenye makazi yake, mjini Morogoro.

“Waliagana, jamaa akaondoka. Kufika mapokezi aliamua kulipa chumba hicho. Mhudumu akamwambia sawa umelipa chumba chenu, mbona chumba cha dereva bado?

“Jamaa akashtuka! Akamuuliza mtu wa mapokezi, dereva gani? Akajibiwa mkewe alichukua vyumba viwili, cha kwako na cha mtu aliyesema ni dereva wake.”

MUME ATAKA JINA
“Mhudumu bila kufumbafumba macho, akamwonesha kitabu cha mapokezi mume, akaona jina la huyo dereva. Akamwomba mtu wa mapokezi akamwoneshe hicho chumba chenye dereva, akapelekwa.

“Kufika, si akamkuta mwanaume ambaye amekuwa akimtilia shaka siku nyingi kwamba ana uhusiano usiofaa na mke wake.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com