Habari Njema Shinyanga na Simiyu!! MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YAANZA KUFANYA KAZI RASMI



Jengo la mahakama kuu Kanda ya Shinyanga lililopo mjini Shinyanga karibu na Kituo cha Mabasi -Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Kaimu jaji mfawidhi mahakama kuu kanda ya Shinyanga Amir Mruma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi ambapo
amesema shughuli za mahakama kisheria katika mahakama hiyo zimeanza mwezi Julai mwaka huu,lakini kutokana na kutokamilika kwa miundo mbinu kesi zimeanza kusikilizwa mwezi Novemba 2015 na wanategemea kupata kesi nyingi za madai,jinai ,ardhi na nyinginezo kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu ambayo awali wananchi walikuwa wanalazimika kwenda mkoani Tabora kufungua kesi na kujikuta wakitumia gharama kubwa kwenda kwa ajili ya kesi zao.


Jaji Mruma amesema Mahakama ya kanda ya Tabora ilikuwa na mikoa minne ambayo ni Tabora,Kigoma Shinyanga na Simiyu na kufuatia kuanzishwa kwa mahakama kanda ya Shinyanga kesi zote zilizokuwa zinasikilizwa Tabora zitahamia mahakama kanda ya Shinyanga inayojumuisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.


Kuwepo kwa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga kutasaidia kupunguza kero ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kimahakama katika mahakama kuu kanda ya Tabora.Kwa mujibu wa Jaji Mruma
tayari zaidi ya kesi 100 zimehamishwa kutoka mahakama kuu kanda ya Tabora na kuletwa mahakama kanda ya Shinyanga,na wamepokea kesi moja inayohusu mambo ya uchaguzi mkuu 2015.


Naibu msajili wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi ofisini kwake ambapo amesema wameanza kupokea kesi tangu tarehe 02 Novemba 2015 na kesi zimeanza kusikilizwa tangu tarehe 12,2015 hivyo kutumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa mikoa ya Shinyanga na Simiyu kufika katika mahakama hiyo badala ya kusumbuka kwenda Tabora.


Naibu msajili wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje amesema tayari mahakama hiyo ina majaji wawili ambao ni jaji Samir Mruma na jaji Victoria Makani ambao wanaendelea kusikiliza mashauri yaliyofika kwa rufaa baada ya kusikilizwa katika mahakama za chini na yale yanayoanzia katika mahakama hiyo moja kwa moja na kuongeza kuwa Novemba 12,2015 wamesikiliza kesi 6 na leo Novemba 13,2015 kesi 8.


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post