Mchezo wa pili wa michuano ya Kombe la CECAFA Challenge Cup 2015 kwa siku ya leo ya November 22 umemalizika kwa kuzikutanisha timu ya taifa ya Uganda dhidi ya Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Kenya Harambee Stars, huu ukiwa ni mchezo wa kwanza wa michuano hii kwa pande zote mbili.
Uganda ambao wanafahamika kwa uwezo wao mzuri uwanjani walishindwa kutamba mbele ya Kenya kwani walikubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo, pamoja na kuwa timu ya taifa ya Kenya inatajwa kukumbwa na tatizo la kiuchumi lakini ilifanikiwa kufanya vizuri.
Matokeo ya mechi za November 21 na 22 na ratiba ya mechi za November 23 na 24.
Mchezo ambao ulianza kwa kila timu kuanza kwa kusoma mchezo wa mpinzani wake, ilichukua dakika 29 za mwanzo Kenya kuweza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Jacob Keli, Kenya walienda mapumzika wakiwa mbele kwa goli moja na kipindi cha pili kilianza kwa kumuingiza Michael Olunga ambaye alienda kuongeza goli la pili dakika ya 50 na kuwafanya Uganda kuondoka uwanjani vichwa chini.
Social Plugin