Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amemteua Dk. Tulia Ackson Mwansasu kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutengeua nafasi yake ya awali aliyokuwa akishikilia kama Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Mh. Dk Tulia anakuwa Mbunge wa kwanza wa kuteuliwa na Rais, kumbuka pia Dk. Tulia ni mmoja kati ya watu watatu waliopitishwa na CCM kuwania nafasi ya Spika wa Bunge
Social Plugin