Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JINSI WAZIRI MKUU MPYA WA TANZANIA MH MAJALIWA ALIVYOTOA MACHOZI LEO


Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa, amesema hakuwa na taarifa yeyote juu ya uteuzi wake uliofanywa na Rais na John Pombe Magufuli.


Akizungumza na Azam TV, Mheshimiwa majaliwa amedai usiri uliotumika ni mkubwa ambao hata yeye atauendeleza katika kuimarisha Serikali.


“Huwezi amini mpaka asubuhi nafanya zoezi na Wabunge wenzangu sikuwa najua lolote, mimi ni kocha wa timu ya mpira ya Bunge.


"Yaani mpaka Spika ameanza na ile Ruangwa nikapigwa na butwaa, na nimelia kwa sababu sikuamini kilichotokea, ila ndo hivyo Rais ameniamini akanipa nafasi” alisema Mh. Majaliwa.


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,leo mchana Limempitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri mkuu mpya.


Kuthibitishwa kwa uteuzi wake kumetokana na kura za ndio na hapana zilizopigwa na wabunge.


Mh. Majaliwa amethibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu mteule kwa kupata kura za ndio 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote 351 zilizopigwa.


Kura za hapana ni kura 91 sawa na asimilia 25 ya kura zote, na kura zilizoharibika ni 2.


Majaliwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini na ameahidi kuwatumikia watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amemteua mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.


Uteuzi huo umetangazwa Bungeni leo na spika wa bunge, Job Ndugai aliyesoma barua iliyoandikwa kwa mkono na Rais Magufuli.


Kabla ya hapo, mh Majaliwa alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI).


Bunge limesimama kwa muda kupisha mchakato wa wabunge kuthibitisha uteuzi huo.


Mheshimiwa Majaliwa alizaliwa December 22, 1960.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com