Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hatari!! KAKA AUA MDOGO WAKE BAADA YA KUMKUTA AKIFANYA MAPENZI NA NGURUWE



MTOTO wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa mkoani Njombe Simon Dastani amefariki dinia baada ya kupigwa kwa fimbo na kaka yake baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe mali ya mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa kijana huyo aliuawa baada ya kaka yake kusikia kijana huyo ameidhalilisha familia yao kwa kufanya mapenzi na mnyama na kuanza kumchapa fimbo kitu kilicho sababisha kutoka damu nyingi na kupelekea kifo chake.

Alisema kuwa katika tukio hilo kaka wa marehemu, Sylvester Dastani alikimbia baada ya kuona hali ya ndogo wake kuwa mbaya na kuwa jeshi la polisi mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi wanamtafuta kijana huyo ili kumtia hatiani.

Alisema kuwa kaka huyo aliamua kuchukua hatua ya kumpiga na fimbo ndogo wake baada ya kuona ameidhalilisha familia yao na baada ya kumchapa na fimbo alimfunga na kamba kijana huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com